Vanuatu yaadhimisha sherehe za miaka mia mbili kwa mradi wa huduma Huko Port Vila, Vanuatu, marafiki, majirani, na maafisa wa serikali walifanya usafi wa kando ya mto na mradi wa upandaji kuadhimisha sherehe za miaka mia mbili . Kundi lilijaza mifuko 100 kwa matakataka waliyokusanya kando ya mto na kupanda majani na miti kadhaa kuzuia mmommonyoko wa udongo.