Vijana washiriki kurembesha ujirani kabla ya sherehe ya miaka mia mbili Kundi la vijana huko Istanbul, Uturuki, lilikuja pamoja kwa ajili ya kuchora picha ya rangi juu ya ukuta wa jengo moja katika ujirani wao, wakiwahamasisha wengine katika eneo hilo kuchangia katika urembeshaji wa mazingira yao. Akielezea kusudi la mradi, kijana mmoja alisema kuwa, ”Sisi tulifanya mradi huu kwa ajili ya kuinua utambuzi katika jimbo letu kuhusu umuhimu wa kutoa huduma pamoja.”