close

Uholanzi

Vijana Uholanzi wakiweka Maneno Yaliyofichwa ya Bahá’u’lláh kwenye muziki
Huko Uholanzi, vijana na watu wazima wamekuwa wakiongeza nguvu kwenye shughuli zao katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye sherehe za miaka mia mbili kama sehemu ya mpango wa Kiangazi cha Huduma. Katika video hii, baadhi ya washiriki wameweka kwenye muziki mateuzi kutoka moja ya Maneno Yaliyofichwa ya Bahá’u’lláh: "Inua kichwa chako kutoka usingizini, kwa maana Jua limechomoza na kupanda hadi kichwani, huenda likakuangazia nuru ya uzuri."