Brazil

Sherehe kutoka kote ulimwenguni

Hapa chini ni dondoo za sherehe zilizofanyika kuenzi miaka mia mbili ya kuzaliwa kwa Báb kwenye maeneo mbalimbali nchi nzima

Brazil

Nakala ya gazeti imeleta mwanga katika jitihada za jamii ya Kibahai katika kuchangia kwenye jumuiya

Gazeti kubwa la kila wiki, lilichapisha nakala kuhusu jamii ya Wabahai wa Salvador, Brazil, pamoja na sherehe zijazo za miaka mia mbili. Nakala ilijadili jinsi gani jamii ya Kibahai ianavyolenga kuweka imani zake katika vitendo, ikigusa kanuni kama umoja wa wanadamu na jitihada za sasa za kuchangia katika maendeleo ya jamii yao. Nakala pia ilionyesha sehemu ya jamii katika historia ya Imani, ikielezea kuwasili kwa Martha Root, muumini mashuhuri wa mwanzo wa Kibahai, huko Bahia mwaka 1919.