Onesho la Kisanii laonesha mchoro uliopata uvuvio kutokana na sherehe za miaka mia mbili
Onesho la kisanii huko Montreal, Canada, laonesha tafakari ya msanii mmoja, iliyowasilishwa katika michoro, juu ya maisha na mafundisho ya Báb. "Nimekuwa daima nikivuviwa sana na (maandiko ya awali ya Báb), jinsi kaligrafia hiyo ilivyowekwa katika ukurasa, na maelezo katika mstari," msanii alieleza. Kazi zimepata uvuvio kutokana na dhana tofauti, kama vile kumuabudu Mungu na uhusiano kati ya akili na roho.