Watoto wafanya mazoezi ya igizo kuhusu ushujaa
Kama mojawapo ya sehemu ya sherehe zao za miaka mia mbili, kikundi cha watoto huko Misri walifanya mazoezi ya igizo lilohamasishwa na hadithi ya Quddus, ambaye alikuwa wa mwisho katika ya Herufi za Uhai - jina waliopewa wafuasi 18 wa Bab ambao kila mmoja wao bila utegemezi aliweza kumtambua Yeye. Quddus, mwenye umri mdogo kati ya kundi lote, alionyesha hali ya ibada na ujasiri iliyomfanya kuwa mwanafunzi wa mbele kabisa wa Bab. Watoto hawa, ambao waliigiza, ni sehemu ya madarasa kwa mafunzo ya kiroho na kimaadili