Igizo kuhusu Mkono wa Imani aliyezaliwa Hawaii, Agnes Alexander
Igizo katika shule ya kiangazi huko Honolulu, Hawaii, likisimulia hadithi ya jinsi Mkono wa Imani Agnes Alexander alijifunza na baadaye kukubali Imani ya Kibahai. Bi Alexander alizaliwa Honolulu mwaka wa 1875 na alijifunza kuhusu Imani alipokuwa akisafiri huko Roma, Italia. Alihamia Japan mwaka wa 1914 na alirudi Hawaii mara kwa mara katika miongo mitano iliyofuata, na mwishowe kuaga dunia katika nchi yake ya asili. Shule hii pia ilionyesha igizo lingine kuhusu uhusiano mzuri wa kihistoria: mkutano wa kwanza kati ya Malkia Lili’uokalani, mfalme wa mwisho wa Hawaii, na wabahai wa kisiwa hicho.