Wimbi baada ya wimbi la sherehe la funika pande zote za nchi katika sherehe zilizofanyika wiki nzima
Katika mipangilio isiyohesabika katika pande zote za Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, makumi elfu walikusanyika kuadhimisha sherehe za miaka mia mbili za kuzaliwa kwa Bab. Sanaa zilizochanua kwa sherehe za furaha zikiwa na sifa ya ushirikiano wa kiroho na maelewano. Familia zilifungua nyumba zao kwa majirani na marafiki, jamii zilikaribisha machifu na wazee wa vijiji, na wengi walikutana katika miji kuchunguza mafundisho ya Imani na maana yake katika jamii.
Mawasilisho na majadiliano kuhusu mada kuu za kiroho ziliwahusisha wadogo na wakubwa pia. Kwa mfano, katika shule nyingi za jamii zinazo hamasishwa na Ubahai walimu waliwahusisha watoto kuchukua nafasi yao kama wahusika wanaochangia katika ustawi wa jamii zao. Kati ya vijana, jitihada kubwa, zinazohamasishwa na mashujaa wa mwanzo wa Imani, wanafanywa kuwa wa huduma katika vijiji vya jirani na jamii. Kwa mfano, kujenga na kurekebisha majengo yatayotumika katika sherehe za miaka mia mbili. Hali hii pia inaenezwa kupitia idadi kubwa ya ripoti za vyombo vya habari kuhusu sherehe hizi nchini kote.
Kutokana na hii, idadi kubwa pande zote za nchi inahamasishwa kuchangia katika mabadiliko ya kimwili na ya kiroho ya jamii yake.