Jamii huko Indonesia yasherehekea kwa maonyesho ya mabango
Katika kuadhimisha sherehe za miaka mia mbili ya kuzaliwa kwa Bab, kikundi cha marafiki huko Bali, Indonesia, waliandaa maonyesho kuhusu historia ya Imani ya Kibahai na baadhi ya mafundisho yake. Sherehe zilianza kwa kusoma sala kutoka dini tofauti, zikifuatiwa na maonyesho ya sanaa kutoka kwa baadhi ya vijana, na uonyeshaji wa filamu Alfajiri ya Mwanga. Maonyesho yalichechemua maongezi ya maana kati ya washiriki.