Kughani sala za Báb kwa Kiarabu
Mbahá’í kutoka Kuwait aliandaa rekodi ya ughani wa sala kadhaa za Báb, ikiwemo teuzi kutoka ifuatayo: “Umetukuzwa sana Wewe, Ee Bwana! Tulinde sisi kutoka kile kilicho mbele yetu na nyuma yetu, juu ya vichwa vyetu, upande wetu wa kulia, upande wetu wa kushoto, chini ya miguu yetu na katika kila upande mwingine ambao tumeachwa wazi. Hakika, wewe u Mlinzi juu ya vitu vyote bila kushindwa.”