Watoto, vijana, na watu wazima wanajiandaa kwa ajili ya sherehe za miaka mia mbili huko Tajikistan
Ni miezi sasa, watoto, vijana na watu wazima kutoka pande za Tajikistan wamekuwa wakijitahidi kuendeleza mafunzo yao yenye lengo la kujenga uwezo kwa ajili ya huduma. Kutokana na mikusanyiko hii, maandalizi ya sherehe za miaka mia mbili yamekuwa yakifanyika katika miji tofauti, vijiji, na ujirani. Jamii nyingi zimekuwa zikionyesha filamu Alfajiri ya Mwanga —hadi kufika kwenye sherehe. Mikutano tofauti kwa ajili ya kusherehekea sherehe za miaka mia mbili imekuwa ikifanyika.