Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

Dansi kuonesha mafundisho ya Bahá’u’lláh

Katika mji wa Sulaymaniyah- mji ambao Bahá’u’lláh alitembelea wakati wa miaka miwili aliyoishi Kurdistan - watu wa jamii hiyo walisheherekea sherehe za miaka mia mbili kwa kucheza dansi iliyoitwa "Mtume" ambayo ilifundishwa na msanii maarufu. Dansi hiyo ilirekodiwa na kuoneshwa kwenye televisheni kuwaburudisha wengi.