Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

Filamu fupi 95 katika siku 95

Huku Ireland, jamii ya wa-Bahá’í ilitengeneza filamu fupi 95, kila siku, hadi kufikia sherehe za miaka mia mbili. Filamu zilizopo hapa zinasimulia matukio mafupi ya maisha ya Bahá’u’lláh na yanaonesha baadhi ya Maandiko yake kwa ubunifu.