Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

Hadithi za Bahá’u’lláh zikihadithiwa kwa lugha tofauti

Kikundi cha marafiki kutoka Tshwane, Afrika ya Kusini, walitengeneza video kwa ajili ya miaka mia mbili. Video hizo ziliwaonesha wakiwa wanahadithia hadithi, kila moja ilionesha upendo wa pekee kwa Bahá'u'lláh, kwa lugha tofauti.