Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

Igizo likonesha matukio kutoka maisha ya Bahá'u'lláh

Kutoka na shauku ya moyoni ya kushiriki na marafiki na familia ujumbe juu ya maisha ya Bahá'u'lláh, kikundi cha vijana wadogo kutoka mji wa Pune waliamua kuandaa igizo. Miezi michache iliyopita, waliandaa igizo na walilifanyia kazi na mwalimu wa kucheza muziki alitengeneza dansi. Walialika washiriki kutoka wanafunzi na vijana wadogo na kugundua watu wengi walikua na shauku. Kikundi kilitengeneza roho ya nguvu ya umoja katika tukio hilo, ikitokea mojawapo ya washiriki hakuweza kushiriki kwenye onesho, wengine wangejitoa kusaidia. "Hii hali ya kuwa moja ya kikundi, ambapo kila mmoja hujitoa ili aweze kujitoa kufanya kazi pamoja na kufanya igizo hili liwezekane, ni ajabu sana."