Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

Kaligrafia kutoka Bahrain

Kaligrafia hizi nne ya rangi za mafuta zilitengenezwa kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili ya kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh. Kipande cha kwanza ni kifungu kutoka kwenye mojawapo ya Maandiko Yake : "Shirikiana na dini zote kwa amani na maelewano..."