Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

Kusheherekea kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh Baku

Huko Magomayev Azerbaijan, kwenye ukumbi wa Philhamornic, jioni ya muziki wa classical ulioongozwa na kiongozi wa State Philharmonic Symphony Orchestra, Rauf Abdullayev. Mbali na maonesho ya muziki, wageni walitazama filamu ya *Mwanga wa Dunia*, walishiriki katika sala, na kuburudishwa na chakula na chai, walizungumza juu ya maisha na mafundisho ya Bahá’u’lláh.