Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

Kuwinda hazina huko Copenhagen, Denmark

Uwindaji wa hazina kote katika mji wa Copenhagen, Denmark, uliandaliwa kama sehemu ya sherehe za miaka mia mbili. Picha ziliwekwa maeneo mbali mbali ya majengo ya jiji lote, na, ziliposkaniwa na simu za mikononi, zilionesha kifungu kutoka Maandiko ya Bahá’u’lláh.