Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

Mafundisho ya Bahá’u’lláh yahamasisha maonesho ya kisanii

Kuadhimisha miaka mia mbili ya kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh mchoraji wa rangi wa Kikazakh Lyazzat Serzhan alionesha seti mpya ya michoro ya rangi katika maonesho ya hivi karibuni huko Uralsk, Kazakhstan. Michoro 50 ya rangi ilioneshwa, yote ilitengenezwa ndani ya miezi sita kuenzi miaka mia mbili.