Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

Makusanyo ya nyimbo yaliyotokana na hamasa ya sherehe za miaka mia mbili

Wakihamasishwa na dhana na vifungu kutoka Maandiko ya Kibahá’í, pamoja na matukio ya kuvutia kutoka katika historia ya Imani, wanamuziki kutoka Spain walikusanya albamu ya nyimbo za maadhimishao ya miaka mia mbili. Nyimbo zilionesha hisia mbali mbali, kutoka shukrani kwa kutimiza utabiri wa dini zilizopita na hamu ya kuleta umoja ulimwenguni.