Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

Maonesho katika miji huko Queensland ikiangalia dhima ya 'nuru' kupitia sanaa

Wasanii kutoka Queensland, Australia, wameshirikiana kuweka maonesho, yaitwayo "niangazie", kuenzi sherehe za miaka mia mbili. Maonesho na natukio yaliyoambatana nayo yalijumuisha muziki, dansi, ushairi, mandala, upakaji rangi, yakihamasishwa na dhima ya "nuru".