Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

Maonesho ya nguo ya tapa iitwayo "Kitu kinafanyika hapa"

Mkusanyiko wa kazi zilizotengenezwa hivi karibuni huko Fiji, zilihamasishwa na maandiko ya ki-Bahá’í na kuoneshwa New Zealand wakati wa kipindi hiki cha kuadhimisha miaka mia mbili. Msanii Dame Robin White alieleza kuwa maandiko ya Bahá’u’lláh yamejaa mifano inayoweza kutafsiriwa katika picha zenye kueleza maana.