Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

Maonesho ya sanaa mitaani huko Greifswald, Ujerumani

Maonesho ya sanaa Greifswald, Ujerumani, yatafunguliwa kwa watu wote mwezi wa kumi. Wakazi wengi wa Greifswald walialikwa katikati ya mji kuchangia katika kuchora michoro miwili ambayo yatakuwa mojawapo ya maonesho.