Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

Maonesho yakusisimua yafanyika Frankfurt

Katika wiki ya kwanza ya Oktoba, ukumbi mkubwa kwenye jengo maarufu huko Frankfurt lilionesha maonesho ya maisha ya Bahá’u’lláh. Jamii ya Wa bahá’í walikabidhiwa ukumbi huo na ofisi ya meya, pamoja na kuangalia picha, wageni walikaribishwa katika mkutano wa ibada kila mwisho wa siku. Maonesho yalivutia watu 27,000.