Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

Mchoro wa rangi ukiwakilisha "Miangaza Pacha" Báb na Bahá’u’lláh

Maduara mawili ni tabia ya Jua kwenye upeo wa macho ukiwaelekeza wanadamu kwenye mwangaza, kila kimoja kinajumuisha kipande cha historia ya ki-Bahá’í. Rangi ya buluu inawakilisha bahari kubwa sana ambapo baba yake Bahá’u’lláh aliota ndoto ya Bahá’u’lláh na samaki katika nywele zake na ya kijani imetokana na kilemba alichovaa Báb akiwa kijana mwangavu.