Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

Mti wa mzeituni wapandwa Albania

Kama mojawapo ya sherehe za miaka mia mbili ya kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh, kikundi cha watoto na vijana, pamoja na walimu wao, wazazi, na marafiki walipanda mti wa mzeituni karibu na shule ya jirani karibu na Tirana, Albania.