Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

Muziki waijaza sherehe huko Uturuki

Katika nyumba na senta Uturuki yote, muziki na maandiko na nyimbo za maandiko matakatifu zilizijaza sherehe na roho ya kipekee. Wimbo wa utamaduni wa Kituruki, au "turku", ulitungwa kwa ajili ya maadhimisho katika mji wa Sivas.