Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

Nyimbo za Kibahasa Indonesia

Wanamuziki wawili wakiimba maneno yafuatayo ya Bahá’u’lláh: "Uzuri wa Kale amekubali kufungwa minyororo ili wanadamu waweze kufunguliwa kwenye utumwa wao, na amekubali kuwekwa mfungwa ndani ya Ngome hii ya Nguvu ili ulimwengu wote uweze kufikia uhuru wa kweli...Tumekubali kujiweka chini, Enyi waumini wa Umoja wa Mungu, ili muweze kutukuzwa, na tumeteseka kwa mateso makubwa, ili muweze kunufaika na kukua."