Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.
Nyimbo hizi za Kibslama zilitungwa kusherehekea miaka mia mbili ya kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh mwaka huu. Wa kwanza ni kutoka kwa waimbaji wa New-Era Radiant uitwao "Kwa Bahá’u’lláh" unaohusu kutafuta na kumpata Yule Aliyeahidiwa. Wa pili ni kutoka kwa Joel Malisi unaomhusu Bahá’u’lláh kuja kuunganisha wanadamu.