Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

Picha iliyochorwa ukutani na vijana wa Moldova

Baadhi ya watoto na vijana walitengeneza picha zilizochorwa ukutani katika kuta zilizochaguliwa zikiwa na vifungu kutoka maandiko ya ki-Bahá’í katika maandalizi ya sherehe za miaka mia mbili. Picha iliyochorwa ukutani 1 - "Acha matendo na si maneno yawe pambo lako" Picha iliyochorwa ukutani 2 - "Acha moyo wako uwashwe kwa upendo wa wema"