Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

Picha zilizopakwa rangi kwenye ukuta Avondale

Watu 100 walishirikiana na shule ya mtaani kupaka rangi nzuri kwenye ukuta kusheherekea utofauti. Hizi rangi za kupaka ukutani zitaoneshwa wakati wa sherehe za miaka mia mbili za jamii ya Avondale, kitongoji cha Auckland, New Zealand. Kulikuwa na kuta tisa, ikijumuisha mifumo iliyotengenezwa na wanafunzi zaidi ya 100 na walimu. Picha za ukutani zinagusia mada ya umoja, familia na upendo.