Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

Sala zatafsiriwa, kuwekwa kwenye muziki, katika lugha ya Kicorsica kwa mara ya kwanza

Huko Corsica, kisiwa katika bahari ya Mediterranean huko kusini mashariki mwa Ufaransa, kitabu cha sala kimechapishwa kwa ajili ya kuadhimisha sherehe za miaka mia mbili, mara ya kwanza Maandiko ya Kibahá’í yalitafsiriwa katika lugha ya asili. Kichapisho kinajumuisha sala 67 na maandiko. Sala mbili ziliwekwa katika muziki na kuimbwa na mtunzi maarufu wa Corsican.