Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

Sanaa ya kaligrafia kutoka UAE

Katika roho ya kusherehekea sherehe za miaka mia mbili, kikundi cha watoto Dubai, kutoka Muungano wa Nchi za Kiarabu, walikusanya sanaa mchanganyiko za kupaka rangi. Kifungu kutoka maandiko ya Bahá’u’lláh kilisomeka "wote waliumbwa kwa maelewano na muungano", ikiwa imeandikwa kwa kaligrafia ya Kiarabu.