Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

Sherehe za dansi Bronx, Mji wa New York

Eneo la Bronx katika mji wa New York ni eneo lenye vitongoji vilivyoshamiri na sehemu ambayo muziki wa hip hop ulianza kuanzia miaka ya sabini. Muziki wa hip hop, mchanganyiko wa muziki wenye midundo na mashairi ya kufoka foka, uliwapa muonekano wa kisanii watu ambao bila muziki huo wasingeweza kuwa na muonekano huo. Muziki, muhimu sana katika sehemu hii ya mji, bila shaka umekua pia mojawapo ya sherehe. Kwa roho hiyo, jamii ya ki-Bahá’í ya Bronx, ikishirikiana na nyumba ya sanaa ya makumbusho ya Bronx, walifanya sherehe kuashiria tukio la miaka mia mbili ya kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh. watu wa umri wote na wenye kutoka sehemu tofauti walihudhuria. Wageni pia walipata fursa ya kuangalia michoro ya rangi iliyohamasishwa na maisha ya Bahá’u’lláh.