Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

sherehe zahamasisha uchongaji wa kinyago cha Kimāori

Kikundi cha vijana wadogo wa kitongoji cha Somerfield cha Christchurch walishirikiana na marafiki wenye ujuzi wa Tikanga Māori kubuni pou - kinyago cha utamaduni cha Kimāori. Vijana walimtuma mchongaji wa eneo hilo aliyetengeneza mhimili wa mātai iliyotengenezwa upya kufuatana na mchoro, wakiwa wanasoma hadithi kutoka maisha ya Bahá’u’lláh. Sanamu hiyo iliwekwa kando ya mti wa asili uliopandwa na jumuia kuadhimisha sherehe huko katika hifadhi za Ernle Clark wakati wa sherehe kama mojawapo ya sehemu ya maadhimisho.