Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

Tamasha la kwaya la wa-Bahá’í wa Australia katika Nyumba ya Ibada huko Sydney

Tarehe 10 na 11 Septemba, washiriki themanini kutoka maeneo tofauti ya maisha walionyesha muziki wa kwaya katika tamasha maalum la miaka mia mbili lililofanyika katika Nyumba ya Ibada ya Ki-Bahá’í huko Sydney. Tamasha lilileta watunzi tofauti, ambao kazi zao zilisherekea maisha na ujumbe wa Bahá’u’lláh. Watu 1,500 walihudhuria maonesho. Dhima kuu ya tamasha ilikua ni uhusiano mkuu kati kumuabudu Mungu na huduma kwa jamii.