Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

Uchongaji wa mbao ukiashiria umoja katika utofauti

Msanii maarufu kutoka mji uitwao Castel d’Ario, Italia, alichonga ubao uliotengenezwa kwa picha zilizounganishwa kwa dhima ya umoja katika utofauti na kwa maisha ya Bahá’u’lláh. Wakazi katika mji walikaribishwa kupaka rangi ubao katika eneo la wazi ambapo waliweza kujifunza kuhusu sherehe za miaka mia mbili. Kazi ya mwisho ya sanaa, ilioneshwa karibu na nyumba ya serikali ya mtaa, ilitokana na juhudi za pamoja. Kupitia mchakato ambao ilitengenezwa na dhima iliyokuwa ikionyesha, sanaa hii iliashiria umoja katika utofauti.