Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

Uchongaji wa mbao uliotengenezwa kwa ajili ya sherehe za miaka mia mbili

Wa-bahá’í wa Duncan, mji uliopo mabonde ya Cowichan kwenye kisiwa cha Vancouver, waliwasilisha benchi maalumu lilichongwa katika sherehe ya kiutamaduni ya Cowichan sherehe ilyofanyika katika nyumba ya wazee (Ts'i'ts'uwatul' Lelum) katika hifadhi ya Cowichan. Wakowichan ni watu wa asili huko magharibi ya Canada. Benchi la njano la seda, lilichongwa na mchongaji Trevor Husband, linaonesha ndege aina ya tai aliyechongwa kwa ugumu mwenye kuashiria ishara muhimu kwa tamaduni za watu wa Cowichan na kwa Maandiko ya ki-Bahá’í. Maandiko yafuatayo ya Bahá’u’lláh yamechongwa kwa juu na chini ya tai kwa lugha ya Hul’q’umi’num na kwa kiingereza "Mwanga wa umoja ni wenye nguvu zaidi kwamba unaweza kufunika ulimwengu wote"