Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

Utunzi wa mwanzo wa igizo linalomhusu Bahá’u’lláh

Miziki hii ya vyombo vitupu ilitungwa na Nikolaï Clavier kwa ajili ya igizo la sinema iitwayo " Mlipuko wa Tarumbeta", iliwakilisha sampuli za nyimbo zitakazochezwa wakati wa sherehe zijazo za miaka mia mbili huko Norway. Kila kipande kitaonesha kipande kutoka katika maisha ya Bahá’u’lláh duniani, na pia kumtukuza ikiambatana na vifungu na majadiliano kwenye igizo la sinema. Wa kwanza unaitwa "Mlipuko wa Tarumbeta", wa pili ni "Mjakazi wa Mbinguni", wa tatu ni "Rizvani", na wa-nne ni "Uhamisho" na watano ni "Kufia dini kwa Badi".