Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

'Uzuri wa Kale', albamu ya nyimbo

Albamu hii, ilitengenezwa na Elika Mahony, inahusisha mpangilio wa muziki na Maandiko ya Bahá’u’lláh kwa kinanda, chelo, santuri na gitaa. Kifuniko cha album kilikatwa vizuri kwa leza iliyotengenezwa kwa kufananishwa na geti la ndani la kuingilia Kaburi la Bahá’u’lláh na albamu inajumuisha utambulisho mfupi ulioandikwa juu ya Maisha na Ujumbe wa Bahá’u’lláh.