Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

Video ya muziki ya vijana wa Chuquisaca, Bolivia

Vijana kutoka eneo la milima ya Andes ya Bolivia waliunda kikundi cha muziki kiitwacho Mianga ya Miongozo na kutengeneza DVD yenye video sita kuadhimisha miaka mia mbili ya kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh. Waliandika: "Tunatoa wimbo huu kwa sherehe za miaka mia mbili ya Uzuri Uliobarikiwa kwa upendo wetu wa kweli. Shauku yetu ya ndani ni kuwa wimbo huu ufikie mioyo ya watu na hisia za watoto, vijana chipukizi, vijana, familia, jamii na watu wote na tunatumaini na serikali"