Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

Vifungu kutoka sala ya ‘Abdu’l-Bahá vikiwekwa katika muziki na jamii ya wa-Bahá’í wa Ukraine

Vifungu kutoka katika sala ya ‘Abdu’l-Bahá vikisomeka kama ifuatavyo: E Mungu! Wewe U mkarimu kwa wote, wewe umewapa wote, wewe umewapa makao wote, umewapa maisha wote. Wewe umewajalia wote na vipaji na stadi, na wote wamezamishwa katika Bahari yako ya Rehema. Ewe Bwana mwema! Unganisha wote. Acha dini zote zikubaliane na ufanye mataifa yote kuwa moja, ili kwamba wajione kama familia moja... E Mungu! Nyanyua juu bendera ya umoja wa binadamu. E Mungu! Anzisha Amani Kuu Kabisa. Unganisha, E Mungu, mioyo pamoja. Ewe Baba mwenye ukarimu, Mungu! Furahisha mioyo yetu kupitia manukato ya Upendo wako.