Maonesho Ya Kisanii

Sampuli ndogo kutoka miongoni mwa maonesho ya kisanaa yasiyohesabika yalioandaliwa na watu binafsi na jumuiya mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya tukio la miaka mia mbili tangu Kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh.

Wafungwa wa dhamira wa Iran walifuma mfumo mzuri wa hariri

Kikundi cha wanawake watano wafungwa na wafungwa wengine watano wa dhamira walitengeneza mfumo mzuri wa hariri nyeupe ikiadhimisha ukuu wa miaka mia mbili ya kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh. Walitumia mfumo huo kutenegeneza mpangilio wa picha kuipa sauti hisia zao katika kipindi hiki muhimu.