Mafundisho ya Baha’u’llah katika vitendo

Toka mwanzo wa Imani ya Kibaha’i katika karne ya kumi na tisa, idadi inayokua ya watu wameona mafundisho ya Baha’u’llah yakitoa dira inayovutia ya uboreshaji wa dunia. Wengi wa wamevutiwa na umaizi toka mafundisho haya—umoja wa binadamu, usawa kati ya wanawake na wanaume, uondoaji wa chuki, upatano wa sayansi na dini—na wameweka jitihada kuweka katika vitendo kanuni za Kibaha’I katika maisha na kazi zao.

Wakivutiwa na kanuni ya umoja wa jamii ya binadamu, wabaha’i huamini katika uendelezo wa pamoja wa ustaarabu wa duniani wa kimwili na kiroho utahitaji mchango wa fikra za kina wa watu binafsi wasiohesabika, makundi, na asasi, kwa vizazi vijazo. Jitihada za jumuiya ya Kibaha’i kuchangia katika mchakato huu huonekana leo katika jamii toka pande zote za dunia na zinakaribisha ushiriki wa wote.

Katika kiini cha jitihada za Wabaha’i ni mchakato endelevu wa ujengaji wa jamii ambayo hutaka kuendeleza aina ya maisha na mifumo ya kijamii iliyojengwa juu ya msingi wa umoja wa binadamu. Moja ya jitihada hizo ni mfumo wa elimu ambao umekua kwa hali ya uhalisia kutoka maeneo ya kijijini na ya mjini toka pande za dunia. Nafasi zimeandaliwa kwa ajili ya watoto, vijana, na watu wazima kudadisi mitazamo ya kiroho na kujenga uwezo kuyaweka katika vitendo katika mazingira yao ya kijamii. Kila roho inakaribishwa kutoa mchango wake bila kujali tabaka, jinsia ama itikadi. Jinsi maelfu na maelfu wanavyoshiriki, wanapata umaizi kutoka vyote viwili sayansi na urithi wa kiroho wa watu wa dunia na kutoa mchango kwa ajili ya muendelezo wa maarifa mapya. Muda unavyoenda, uwezo wa kutoa huduma hujengwa katika maeneo tofauti tofauti duniani na huibua jitihada za mtu mmoja mmoja na vitendo vinavyoongezeka ugumu kwa ajili ya uboreshaji wa jamii. Mabadiliko ya mtu binafsi na ya jamii hutokea kwa wakati mmoja.

Zaidi ya jitihada za kujifunza ujengaji jamii katika ngazi ya chini, wabaha’i hushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii, ambamo wanaweka jitihada kuweka katika vitendo kanuni za kiroho kwenye shughuli zenye nia ya kuleta maendeleo ya kimwili katika mazingira tofauti tofauti. Asasi za Kibaha’i na mawakala, pamoja na watu binafsi na mashirika, pia hushiriki katika majadiliano yaliyoenea katika nafasi mbalimbali, kuanzia mazingira ya kitaaluma hadi yale ya kitaalamu, toka mijadala katika ngazi ya kitaifa hadi ya kimataifa, zote zikitoa mchango kwa ajili ya maendeleo ya jamii.

Jinsi wanavyofanya hii kazi, wabaha’i wapo makini kwamba kushikilia mitazamo ya juu (ya kiroho) sio sawa na kuiishi. Jamii ya kibaha’i hutambua kuwa kuna changamoto nyingi zilizo mbele yake wakati wakishirikiana na wengine bega kwa bega kwa ajili ya umoja na haki. Imeshikilia katika lengo la muda mrefu la kujifunza kupitia utendaji ambalo jukumu hili huhitaji, ikiwa na Imani kuwa dini ina nafasi ya muhimu katika jamii na ina nguvu ya juu kwa kufichua uwezo wa mtu mmoja mmoja, jamii na asasi.

Maisha ya Baha’u’llah

Kufanywa upya kwa dini

Ufunuo wa Baha’u’llah