Maisha ya Baha’u’llah

Maandiko ya Kibaha’i mara nyingi hulinganisha ujio wa Mdhihirishaji wa Mungu na mapambazuko ya jua. Kutokea kwa mtume wa Mungu ni sawa na mwanzo wa siku mpya, ambapo miale ya jua hutoa nguvu zake duniani, ikiangazia mwanga kwenye vitu vyote na kuruhusu macho kuona vile vilivyokuwa vimefichwa na giza la usiku.

Siku mpya imewapambazukia watu kwa ujio wa Baha’u’llah, "Utukufu wa Mungu", na Mtangulizi Wake, Bab-Mitume wa Mungu wawili wa karibuni zaidi kati ya Mitume waliowahi kutokea katika historia. Kama vile jua la asubuhi huchangamsha dunia iliyolala kupata uhai, ujio wa Wadhihirishaji hawa Mapacha wa Mungu umetoa nguvu kwa usakaji wa binadamu wa maana za ndani na kusudi la juu la maisha. Mafundisho ya Baha’u’llah yanatoa mwanga kwa shughuli za binadamu wakati ambapo, inaweza kusemwa, giza limetanda duniani. Mafundisho Yake husaidia jamii ya binadamu kupata maana na kuyaendea mabadiliko makubwa ambayo yanatokea kwa kasi. Ingawa mabadiliko haya yanabadili utaratibu wa vitu, yanaleta machafuko, na kuchanganya hata viongozi wenye heshima zao, hufungua njia kwa ajili ya taratibu mpya za maisha na kuibua asasi mpya za kibinadamu.

Katika kipindi hiki chenye misukosuko cha historia ya binadamu, dunia ina hitaji la dira inayounganisha asili yetu ya ukweli kama binadamu na aina ya dunia ambayo tungependa kuishi ndani yake. Wabaha’i huamini kuwa dira hii imefunuliwa katika maandiko ya Baha’u’llah, ambaye maisha na mafundisho Yake ni hadithi yenye mvuto Zaidi wa kipindi chetu.

Filamu fupi: Tafakari fupi juu ya wazo la Wadhihirishaji wa MunguDOWNLOAD

Baha’u’llah alifikisha ufunuo mpya toka kwa Mungu. Dhamira Yake ilikuwa ni uamshaji wa kiroho wa jamii ya binadamu na kuunganisha watu wote wa ulimwengu. Mafundisho ya Baha’u’llah hufanya msingi wa Imani ya Kibaha’i na hutoa muono wa matumaini yasiyo na mipaka na uponyaji. "Lengo langu halikuwa zaidi bali uboreshaji wa dunia na utulivu wa watu wake," aliandika Baha’u’llah. Kwa ajili ya kusudi hili lililotukuka, alivumilia maisha ya mateso, kufungwa, kupewa mateso ya kikatili, na kuhamishwa.

Baha’u’llah, alizaliwa Tehran mnamo Novemba 12, 1817, na alipewa jina la Mirza Husayn-Ali. Baba yake, Mirza Buzurg, alishika nafasi ya juu katika baraza la mfalme wa Uajemi. Akiwa na umri mdogo, Baha’u’llah alionesha sifa ambazo ziliwafanya waliomzunguka kutambua kuwa hakuwa mtoto wa kawaida. Alikuwa na busara na akili za asili, ingawa hakuenda shule yoyote, na aliyozidi kukua, ishara za ukuu Wake ziliendelea kuwa wazi zaidi. Baha’u’llah alijulikana kwa muono Wake wa kina, mwenendo Wake ulioboreshwa, ukarimu na huruma Yake. Akiwa na umri wa miaka 18, Baha’u’llah alimuoa mwanamama mdogo, Navvab, na nyumba yao ikawa ni ngome, sehemu ya mwanga na upendo na ukarimu, iliyo wazi kwa wote.

Nyumba ya Baha’u’llah (kulia) na picha ya mlango wa kuingilia (kushoo) huko Takur, kaskazini mwa Iran, iliharibiwa na serikali ya Iran mnamo 1981.

Baha’u’llah alikuwa na umri wa miaka 22 wakati ambapo baba Yake alifariki, akimuacha Yeye kuwa msimamizi wa mambo ya nyumbani na ya za nyumba za ukoo mzima. Serikali ilimpa Baha’u’llah nafasi ya kiwaziri ya baba Yake, lakini Yeye alikikataa cheo hicho. Hakuwa na shauku na nafasi za juu na sifa; shauku Yake ilikuwa ni katika kutetea maskini na wenye shida. Badala ya kukazania maisha ya nguvu na starehe, Baha’u’llah alichagua kutoa nguvu Zake kwa ajili ya shughuli za usafi wa moyo na matendo ya huduma. Kufikia mwanzo wa miaka ya 1840, alijukana kama "Baba wa Maskini."

Toka wakati Baha’u’llah alipoikubali dini ya Bab, maisha Yake kijana huyu mashuhuri na ya familia Yake yalibadilika kabisa. Bab alikuwa kijana mfanyabiashara wa kutoka Shiraz, Uajemi, ambaye mnamo 1844 alitangaza kuwa Yeye ni mchukuzi wa (mbeba) ujumbe mpya toka kwa Mungu na mtangulizi wa ujio wa Mwahidiwa wa dini zoe. Ingawa Baha’u’llah na Bab hawakuwahi kukutana uso kwa uso, waliwasiliana. Toka kipindi Baha’u’llah alipousikia ujumbe wa Bab, alitangaza Imani Yake kwa moyo wote kwa hoja hiyo na kuweka nguvu na uwezo Wake katika kuitangaza.

Kifungo cha Baha’u’llah kilianzia Uajemi mnamo 1852 ambapo, akiwa kama mfuasi wa Bab, alikamatwa, aliteswa, na kutupwa katika shimo la chini ya ardhi, Siyah-Chal mbaya kabisa ya huko Tehran, "Shimo Jeusi".Ilikuwa wakati wa kifungo hichi, kupitia harufu mbaya ya gereza, uchafu, na giza nene kabisa, ambapo dalili za kwanza za ufunuo mtakatifu zilipomfikia Yeye. Baha’u’llah akiwa amefungwa miguu Yake na shingoni akiwa amezungukwa na mnyororo wa pauni 100, Roho Mtakatifu wa Mungu alifunuliwa Kwake.

Hili lilikuwa ni tukio linalolingana na nyakati maalum za vipindi vya zamani za kale ambapo Mungu alijifunua kwa Mitume Wake wa siku za nyuma: wakati Musa aliposimama mbele ya Kijinga cha Moto; wakati Buddha alipopata mwanga chini ya mti wa Bodhi; wakati Roho Mtakatifu, katika umbo la njiwa, alipomshukia Yesu; na wakati malaika Gabrieli alipomtokea Muhammad.

Katika maandiko Yake, Baha’u’llah baadae huelezea tukio hilo na jinsi ufunuo wa Mungu ulipomfikia:

"Pepo za Aliye-Mtukufu kabisa zilivumishwa juu Yangu, na kunifundisha maarifa ya yale yote ambayo yamekuwepo. Jambo hili halitoki Kwangu, ila kwa Yeye ambaye ni Mweza-Yote na Mjua-Yote. Na aliniamrisha kuamsha sauti Yangu kati ya dunia na mbingu."

"Wakati wa siku nilizokuwa nimelala katika gereza la Tihran, ingawa uzito wa kuelemea wa minyororo na hewa yenye harufu mbaya iliruhusu nipate usingizi mdogo tu, bado katika nyakati hizo chache za usingizi nilihisi kitu kikitiririka kutoka kwenye taji la kichwa Changu hadi juu ya kifua Changu, hata kama mafuriko makali yaliyoshukia duniani toka kilele cha mlima wa juu. Kila kiungo cha mwili Wangu, kutokana na hilo, uliwashwa moto. Katika kipindi hicho ulimi Wangu ulitamka yale ambayo hakuna mtu angeweza kuvumilia kuyasikia"

Alipoachiwa kutoka Shimo Jeusi, Baha’u’llah alifukuzwa toka nchi Yake ya kuzaliwa katika kilichoanzisha uhamisho wa miaka 40, kipindi chote kilichobakia cha maisha Yake duniani. Aliutangazia umma kuhusu ujumbe Wake kama Mtume wa Mungu mnamo 1863.

Kuhamishwa kwa Baha’u’llah
Falme ya Uturuki
huko Persia

Wafuasi wa Baha’u’llah walikuja kujulikana kama Wabaha’i. Jinsi wafuasi hawa walivyozidi kuongezeka, wakivutiwa na sifa Zake zenye mvuto na mafundisho Yake ya kina ya kiroho, Baha’u’llah alizidi kuhamishwa. Alimrishwa kifungo cha jela katika gereza baya kabisa katika himaya ya Uturuki, mji mkongwe wa Akka, uliopo pajulikanapo kama Israel siku hizi. Hali mbaya ya hewa, ukosekanaji wa maji safi, na majengo yaliyoathiriwa na wadudu yalifanya maisha ya Akka kuwa ni adhabu mbaya Zaidi kuweza kutolewa. Baha’u’llah alifika hapo mnamo mwaka1868, akiwa pamoja na wapatao watu 70 kati ya familia Yake na wafuasi Wake. Ilikuwa ni hapo Akka ambapo Baha’u’llah aliandika baadhi ya kazi Zake za umuhimu Zaidi, akiwaandikia wafalme na viongozi wengine wa kipindi Chake, na akifunua sheria na kanuni ambazo zitawaongoza binadamu kuelekea kipindi cha amani ya ulimwengu nzima.

"Dunia ni nchi moja na binadamu raia wake," aliandika. "Mtu asijivunie mwenyewe kwamba anaipenda nchi yake, bora yeye ajisifu kuwa anaipenda dunia nzima."

Jinsi muda ulivyopita, viongozi wa eneo walipunguza makali ya kifungo cha Baha’u’llah na Yeye alihamia umbali kidogo kuelekea kaskazini hadi Bahji, ambapo alitumia miaka 12 ya mwisho wa uhai Wake. Katika kipindi hiki, Baha’u’llah alitembelea mara kadhaa miteremko ya karibu ya Mlima Karmeli ambapo, mnamo mwaka 1891, alichagua eneo la kudumu la kupumzisha mabaki ya Mtangulizi Wake, Bab.

Mnamo 1982, baada ya maradhi ya muda mfupi, Baha’u’llah alifariki akiwa na umri wa miaka 75. Mwili Wake ulihifadhiwa kupumzika katika nyumba ndogo pembeni ya makazi Yake za mwisho ya Bahji. Katika wosia Wake, alimteua Abdu’l-Baha kama mrithi Wake na Kiongozi wa Imani ya Kibaha’i-kwa mara ya kwanza katika historia kwamba Mwanzilishi wa dini ya ulimwengu amemtaja atakayemrithi katika maandishi ambayo hayawezi kubishiwa. Uchaguzi wa mrithi ni kiini wa kile kinachojulikana kama "Agano la Baha’u’llah", likiwezesha jamii ya Kibaha’i kubaki imeungana kwa kipindi chote.

Kaburi la Baha’u’llah

Mafundisho ya Baha’u’llah katika vitendo

Kufanywa upya kwa dini

Ufunuo wa Baha’u’llah