Albamu ya muziki yatengenezwa kuadhimisha sherehe za miaka mia mbili
Katika kuadhimisha sherehe za miaka mia mbili ya kuzaliwa kwa Bab, mwanamuziki huko Macau alitengeneza albamu iliyoitwa Aliyetukuzwa. Ina nyimbo 11 ambazo sala na Maandiko ya Bab yamewekwa katika muziki. jalada la albamu lina rangi ya dhahabu iliyokatwa kwa leza iliyohamasishwa na lango la kuingilia Kaburi Takatifu la Bab.