Wabahai wa Myanmar walitoa heshima katika kaburi la muumini wa mwanzo
Pale mwanzo wa karne ya 20, kijiji chote cha Daidanaw, Mynamar, kikivutiwa na mtazamo wa Bahá’u’lláh kwa ulimwengu ulio wenye msingi wa haki na umoja, kilipokea Mafundisho Yake na kuanza kuyaweka mafundisho katika maisha yao. Abdul-Baha, wakati akiishi Haifa, alifurahi kusikia habari hii na alifananisha Daidanaw kama "kijiji Chake". Mwaka huu, kuadhimisha sherehe za miaka mia mbili, wanakijiji waliikumbuka historia yao, waliungana kusafisha na kupendezesha kaburi la Mkono wa Imani wa Mungu, Siyyid Mustafa Rumi (1846-1945), ambaye alikuwa ni mmoja kati Wabahai wa kwanza huko Myanmar. Siyyid Mustafa Rumi, pamoja na waumini wengine wawili wa mwanzo, waliandaa jeneza la marumaru, lililoamriwa na Abdul-Baha na kujengwa na Wabahai wa nchi hiyo, ambalo lilisafirishwa kwenda Mji Mtakatifu. Jeneza hili la marumaru hivi sasa linahifadhi mabaki matakatifu ya mwili wa Bab.