Mafundisho ya Kibahá’í katika Vitendo

Toka mwanzo wa Imani ya Kibaha’i katika karne ya kumi na tisa, idadi inayokua ya watu wameona mafundisho ya Baha’u’llah yakitoa dira inayovutia ya uboreshaji wa dunia. Wengi wa wamevutiwa na umaizi toka mafundisho haya—umoja wa binadamu, usawa kati ya wanawake na wanaume, uondoaji wa chuki, upatano wa sayansi na dini—na wameweka jitihada kuweka katika vitendo kanuni za Kibaha’I katika maisha na kazi zao.

Wakivutiwa na kanuni ya umoja wa jamii ya binadamu, wabaha’i huamini katika uendelezo wa pamoja wa ustaarabu wa duniani wa kimwili na kiroho utahitaji mchango wa fikra za kina wa watu binafsi wasiohesabika, makundi, na asasi, kwa vizazi vijazo. Jitihada za jumuiya ya Kibaha’i kuchangia katika mchakato huu huonekana leo katika jamii toka pande zote za dunia na zinakaribisha ushiriki wa wote.

Katika kiini cha jitihada za Wabaha’i ni mchakato endelevu wa ujengaji wa jamii ambayo hutaka kuendeleza aina ya maisha na mifumo ya kijamii iliyojengwa juu ya msingi wa umoja wa binadamu. Moja ya jitihada hizo ni mfumo wa elimu ambao umekua kwa hali ya uhalisia kutoka maeneo ya kijijini na ya mjini toka pande za dunia. Nafasi zimeandaliwa kwa ajili ya watoto, vijana, na watu wazima kudadisi mitazamo ya kiroho na kujenga uwezo kuyaweka katika vitendo katika mazingira yao ya kijamii. Kila roho inakaribishwa kutoa mchango wake bila kujali tabaka, jinsia ama itikadi. Jinsi maelfu na maelfu wanavyoshiriki, wanapata umaizi kutoka vyote viwili sayansi na urithi wa kiroho wa watu wa dunia na kutoa mchango kwa ajili ya muendelezo wa maarifa mapya. Muda unavyoenda, uwezo wa kutoa huduma hujengwa katika maeneo tofauti tofauti duniani na huibua jitihada za mtu mmoja mmoja na vitendo vinavyoongezeka ugumu kwa ajili ya uboreshaji wa jamii. Mabadiliko ya mtu binafsi na ya jamii hutokea kwa wakati mmoja.

Katika jumuiya kadhaa, kumeibuka Nyumba za Ibada za Kibaha’i, sehemu kwa ajili ya wote kusali na kutafakari juu ya uhalisia wa kiroho na maswali ya kimsingi ya maisha. Majengo haya matakatifu yapo kwenye jumuiya 10 ulimwenguni, na mengine yanaendelea kujengwa. Mahekalu ya Kibaha’i hufungamanisha sura mbili za maisha zisizoweza kutenganishwa: ibada na huduma. Muungano huu huakisiwa katika mchakato wa muda mrefu wa ujenzi wa jumuiya ambamo, kama Nyumba ya Haki ya Ulimwengu ilivyoandika, “ukuaji wa moyo wa ibada ambao hujidhihirisha katika mikusanyiko kwa ajili ya sala na mchakato wa kielimu ambao hujenga uwezo kwa ajili ya huduma kwa wanadamu.”

Zaidi ya jitihada za kujifunza ujengaji jamii katika ngazi ya chini, wabaha’i hushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii, ambamo wanaweka jitihada kuweka katika vitendo kanuni za kiroho kwenye shughuli zenye nia ya kuleta maendeleo ya kimwili katika mazingira tofauti tofauti.

Uwanda mpana wa shughuli za sasa huanzia kwenye jitihada kutoka vijijini na ujirani hadi kwenye mikoa na mataifa, zikishughulikia mkusanyiko wa changamoto, zikijumuisha elimu kutoka shule ya awali hadi chuo kikuu, ujuzi wa kusoma na kuandika, afya, mazingira, kusaidia wakimbizi, maendeleo ya wanawake, uwezeshwaji wa vijana chipukizi, uondoaji wa ubaguzi wa kimbari, kilimo, uchumi wa mahali, na maendeleo ya kijiji.

Nyumba ya Haki ya Ulimwengu

Asasi za Kibaha’i na mawakala, pamoja na watu binafsi na mashirika, pia hushiriki katika majadiliano yaliyoenea katika nafasi mbalimbali, kuanzia mazingira ya kitaaluma hadi yale ya kitaalamu, toka mijadala katika ngazi ya kitaifa hadi ya kimataifa, zote zikitoa mchango kwa ajili ya maendeleo ya jamii. Michango hii huelezea umaizi kutoka kwenye usomaji wa Ufunuo wa Bahá’u’lláh na huchota kwenye uzoefu wa jumuiya ya Kibahá’í ya ulimwengu. Katika ngazi ya kitaifa, jumuiya zinachangia kwenye mijadala ya maana kama vile usawa wa wanawake na wanaume, uhamiaji na utengamano, jukumu la vijana katika mabadiliko ya kijamii, na upatano wa kidini, miongoni mwa mengine. Na wabahá’í binafsi, Nyumba ya Haki imeandika, “wa rika zote na usuli wanatoa michango yenye thamani kwa mijadala mahsusi, wakileta kwenye utambuzi wa wale wawazungukao mtazamo wa kikanuni uliobumbwa na Ufunuo mpana wa Bahá’u’lláh.”

Jinsi wanavyofanya hii kazi, wabaha’i wapo makini kwamba kushikilia mitazamo ya juu (ya kiroho) sio sawa na kuiishi. Jamii ya kibaha’i hutambua kuwa kuna changamoto nyingi zilizo mbele yake wakati wakishirikiana na wengine bega kwa bega kwa ajili ya umoja na haki. Imeshikilia katika lengo la muda mrefu la kujifunza kupitia utendaji ambalo jukumu hili huhitaji, ikiwa na Imani kuwa dini ina nafasi ya muhimu katika jamii na ina nguvu ya juu kwa kufichua uwezo wa mtu mmoja mmoja, jamii na asasi.