Kufanywa upya kwa dini

Utaratibu wa dini kuu ambao umeiongoza jamii ya binadamu kwa Zaidi ya miaka elfu moja unaweza kuangaliwa kimsingi kama dini moja inayoendelea ambayo hufanywa upya kutoka wakati mmoja hadi mwingine, ukiboreshwa jinis jamii ya binadamu ikitoka hatua moja ya ukomavu/ukuaji wa pamoja hadi nyingine. Dini ni mfumo wa maaria na jinsi ya kuishi ambao, pamoja na sayansi, umesukuma ustaarabu katika historia nzima.

Dini leo haiwezi kuwa sawa sawa kabisa na jinsi ilivyokuwa kwa kipindi kilichopita. Mengi ya yale yanayoaminiwa kuwa dini katika ulimwengu wa kisasa sharti, wabaha’i huamini, kuangaliwa upya kupitia nuru ya ukweli wa msingi ambao Baha’u’llah ameuweka: umoja wa Mungu, umoja wa dini, na umoja wa jamii ya binadamu.

Angalia kwa umakini kuwa katika dunia hii ya kuwa, vitu vyote sharti vifanywe upya daima. Angalia katika dunia ya muumbo iliyokuzunguka, uone jinsi ilivyofanywa upya. Fikra zimebadilika, mfumo wa maisha umefanywa upya, sayansi na sanaa vinaonesha msukumo mpya, uvumbuzi na ubunifu ni mipya, mitazamo ni mipya. Jinsi gani sasa nguvu ya umuhimu kama dini-chombo pekee cha uhakika kwa ajili ya maendeleo ya binadamu, jinsi pekee ya kufikia maisha ya milele, msukumaji usio na mwisho wa ubora, mwangaza wa dunia zote mbili-usifanywe upya?

(Abdu’l-Baha, Mateuzi toka Maandiko ya Abdu’l-Baha,p.56)

Filamu fupi: Tafakari fupi juu ya wazo la Wadhihirishaji wa Mungu

Baha’u’llah aliweka kiwango kisichopingika: kama dini ikiwa ni chanzo cha utenganisho, uadui, au kukosana—mbaya zaidi ugomvi na ugaidi—ni bora kutokuwa nayo. Jaribio la dini ya kweli ni matunda yake. Dini sharti kwa kiwango kinachoonekana iinue jamii ya binadamu, ijenge umoja, ibumbe mienendo mizuri, ihimize utafutaji wa ukweli, kuachia huru dhamiri ya binadamu, kuendeleza haki ya kijamii, na kuhimiza uboreshaji wa ulimwengu. Dini ya kweli hutoa msingi wa maadili kuleta pamoja mahusiano kati ya watu binafsi, jamii na asasi zenye asili mbalimbali na hali yenye mchanganyiko wa kijamii. Huendeleza sifa njema, huingiza uvumilivu, ukarimu, usamehaji, utoaji, na fikra za kina. Hukataza utendaji uovu kwa wengine na hukaribisha roho kufanyiana mema kwa wengine. Hutoa dira inayokumbatia dunia nzima na husafisha mioyo toka fikra za kibinafsi na chuki. Huhimiza roho kuweka jitihada kwa mafanikio ya kimwili na uboresho wa hali ya kiroho kwa wote, kuona furaha yao wenyewe katika furaha ya wengine, kuendeleza ujifunzaji na sayansi, kuwa kifaa cha furaha ya kweli, na kuhuisha mwili wa wanadamu.

Dini hukubali kwamba ukweli ni mmoja, na ndio maana sharti ikubaliane na sayansi. Ikieleweka kamavitu viendavyo sambamba, sayansi na dini huwapa watu jinsi zenye nguvu kupata umaizi mpya na mzuri wa uhalisia na kuibumba dunia inayowazunguka, na kila utaratibu hunufaika kwa kiwango cha kutosha toka mwenzie. Sayansi, bila mtazamo wa kidini, huweza kuathiriwa na taratibu za mambo ya kimwili. Dini bila sayansi huangukia kwenye ushirikina na uigaji bila kufikiria (uigaji pofu) wa zama zilizopita. Mafundisho ya Kibaha’i hufundisha kuwa:

Wekeni Imani zenu zote kukubaliana na sayansi: hakuwezi kuwa na kupishana kwani ukweli ni mmoja. Wakati ambapo dini, ikitenganishwa toka ushirikina, utamaduni, utaratibu usio wa kiakili, na kuonesha ikikubaliana na sayansi, hapo ndipo nguvu iliyounganika kubwa itakapopatikana duniani, isafishayo ambayo itasafisha vita zote, kutoelewana, mafarakano na mivutano-na hapo ndipo jamii ya binadamu itaunganishwa na nguvu ya Upendo wa Mungu.

(Abdu’l-Baha, Hekima za Abdu’l-Baha,p.145)

Dini ya kweli hubadili moyo wa mtu na kuchangia katika mabadiliko ya jamii. Hutoa umaizi kuhusu asili ya ukweli ya mtu na kanuni za jinsi ya kuboresha ustaarabu. Katika hatua hii mahususi ya historia ya binadamu, kanuni ya msingi ya kiroho ya kipindi chetu ni umoja wa jamii ya binadamu. Tamko hili rahisi huwakilisha ukweli wa kina kiasi kwamba, wakati utakapokubalika, litaondoa fikra zote za zamani za kujikweza za tabaka lolote ama taifa. Ni zaidi ya mwito wa kuheshimiana kikawaida na hisia za kutakiana mema katika watu tofauti wa duniani, ingawaje haya pia ni ya muhimu. Ikifanyika hadi hitimisho lake, humaanisha badiliko linalokua katika kila uhusiano wa kijamii na mahusiano ambayo huyadumisha.